Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Mkurugenzi wa Mashtaka

MKURUGENZI WA MASHTAKA

Mkurugenzi wa Mashtaka ni mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Mkurugenzi wa Mashtaka ndiye msimamizi mkuu wa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Mawakili wa serikali na Waendesha Mashtaka katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa ni:

 • (i)Kuamua kushtaki au kutoshtaki kwenye makosa ya jinai;
 • (ii)Kuanzisha, kuendesha na kusimamia mashtaka ya makosa ya jinai katika mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi;
 • (iii)Kutwaa na kuendelea na mashtaka ya kesi yoyote ya jinai iliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine;
 • (iv)Kufuta mahakamani mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine katika hatua yoyote kabla hukumu kutolewa;
 • (v)Kutoa maagizo kwa jeshi la polisi au vyombo chunguzi vyoyote kuchunguza taarifa yoyote ya kijinai na kutoa taarifa kwake haraka inavyowezekana;
 • (vi)Kuchukua hatua muhimu kwa jambo lolote lenyetija katika mashtaka ya jinai;
 • (vii)Kutoa miongozo inayohusu uratibu wa upelelezi na uendeshaji mashtaka;
 • (viii)Kuteua na kutenguamamlaka ya waendesha mashtaka wa umma;
 • (ix)Kumshauri waziri mwenye dhamana katika masualaya mashtaka yanayohitaji sera au hatua za kibunge;
 • (x)Kuteuwa maafisa maalum ndani ya taasisi za serikali kusimamia mali zilizozuiliwa au kutaifishwa na mahakama katika mazingira ambayo ni vigumu kuteua wasii;
 • (xi)Kufanya kazi nyingine ambayo zinahusiana na mashtaka ya umma;
 • (xii)Kuwasimamia maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine walioteuliwa au kuajiriwa na ofisi ya taifa ya mashtaka;
 • (xiii)Kusimamia shughuli zote zinazofanywa na maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka;
 • (xiv)Kuita afisa yoyote wa umma kutoa maelezo au taarifa kuhusiana na jambo lolote ambalo linahusu mashtaka ya umma;
 • (xv)Kuandaa na kuwasilishakwa waziri taarifa ya nusu mwaka na nakala kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya taifa ya mashtaka; na
 • (xvi)Kuteua au kuajiri na kuwajibisha maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka.