Ofisi ya Mashtaka Wilaya ya Nzega
Ofisi ya Mashtaka Wilaya ya Nzega
- Lengo: kutoa huduma za mashtaka kwa umma katika ngazi ya wilaya
- Majukumu:
- Majukumu ya Ofisi ya Mashtaka ya Wilaya ni haya yafuatayo:
- (i)Kutoa huduma zakimashtaka wilayani ikiwa ni pamoja na kufungua, kuendeshaau kuondoa mashtaka yaliyofunguliwa kwa minajili ya kutenda haki, maslahi ya umma na kuzuia ukiukaji wa taratibu za kisheria;
- (ii)Kuratibu upelelezi na kutoa muongozo kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenye makosa ya udanganyifu, rushwa namengine yanayohusiana nayo;
- (iii)Kuandaa hati za mashtaka, maombi na nyaraka nyingine zinazoendeana na haya;
- (iv)Kusimamia kesi za rushwa zinazoshughulikiwa na mamlakanyingine zinazopambana na rushwa na udanganyifu;
- (v)Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi;
- (vi)Kutoa ushauri kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenyemakosa dhidi ya binadamu na mamlaka za umma;
- (vii)Kushughulikia kesi zavifo vya mashaka;
- (viii)Kushughulikiakesi za rufaa na maombi katika mahakama za juu;
- (ix)Kushughulikia mashahidi kabla, wakati wa kusikiliza kesi na baada ya kutoa ushahidi mahakamani;
- (x)Kusimamia kesi zinazohusu makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu na madawa ya kulevya, ndani ya mamlaka yao;
- (xi)Kutoa mwongozo,kufungua na kuendesha kesi zinazohusiana na utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika uhalifu na mazalia yake;
- (xii)Kuratibu kwa kushirikiana na wadau wa haki jinai, kurejesha na kutaifisha mali haramu ndani ya mamlaka yao;
- (xiii)Kuunganisha ofisi ya mashtaka na taasisi nyingine zinazoendesha mashtaka wilayani kwa lengo la kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwa na mwendesha mashtaka;
- (xiv)Kufanya ukaguzi sero za polisi na magereza;
- (xv)Kuwezesha kamati za usimamizi wa uendeshaji kesi katika ngazi ya wilaya na majukwaa mengine;
- (xvi)Kuandaa na kuchambua data za kesi za jinai;
- (xvii)Kutunza kanzi data na mfumo wa taarifa wa mashtaka;
- (xviii)Kuelimisha umma kuhusu uchukuaji na uendeshaji wa mashtaka;
- (xix)Kutekeleza na kusimamia kanuni za nidhamu za waendesha mashtaka
- (xx)Kuratibu uchukuaji wa waendeshaji wa mashtaka toka taasisi chunguzi wilayani;
- (xxi)Kuanzisha na kutunza taarifa za waendesha mashtaka wote wilayani;
- (xxii)Kuratibu na kuongoza taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya mazingira ,kimtandao na makosa mengine yanayoendana na hayo;
- (xxiii)Kusimamia kesi za kimazingira na kimtandao zinazoendeshwa na mamlaka nyingine;
- (xxiv)Kushughulikia maswala ya kiutawala, kifedha nakiutumishi katika mamlaka yao; na
- (xxv)Kufanya utafiti katika masuala ya jinai na uendeshaji wa kesi zake ili kuhakikisha sheria , kanuni ,amri, taratibu na miongozo yote iliyokwishatolewa inafuatwa.
Ofisi ya Mashtaka ya Wilaya, itaongozwa na Afisa Mashtaka wa Wilaya