Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Arusha
MKOA-ARUSHA
Mkoa wa Arusha una ukubwa wa kilomita za mraba 34,515.5 ukiwa na wilaya sita za Karatu, Monduli, Longido, Arusha, Ngorongoro na Arumeru. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 una idadi ya watu 2,356,255. Shughuli kuu za kiuchumi katika Mkoa wa Arusha ni utalii, ufugaji, kilimo na viwanda.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Arusha imeanzishwa mwaka 2018. Ofisi iko katikati ya Jiji la Arusha ambapo tayari Wilaya tano zina huduma za mashtaka. Wilaya hizo ni Karatu, Monduli, Longido, Arusha, Arumeru huku Ngorongoro pekee ikiwa bado haijapata Ofisi ya Mashtaka ya wilaya. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huu ni Kubaka, ujangili, wizi na biashara ya dawa za kulevya.
Anuani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Arusha
S. L P 3144
Eneo/Mtaa -Jakaranda
Barua pepe:arusha@nps.go.tz
Tovuti: www.nps.go.tz