Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Simiyu
MKOA-SIMIYU
Mkoa wa Simiyu ulianzishwa kwa Tangazo la Serikali (GN) Na. 72 la tarehe 02 Machi, 2012. Mkoa wa Simiyu una eneo la kilomita za mraba 23,807.70. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Simiyu una idaidi ya watu 2,140,497. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huo ni Ubakaji, Mauaji na Ujangili. Mkoa wa Simiyu unaundwa na Wilaya tano (5). Shughuli kuu za kiuchumi katika Mkoa wa Simiyu ni utalii, kilimo,ufugaji,uchimbaji madini na Uvuvi.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Simiyu inapatikana katika mji wa Bariadi eneo la Malambo ambapo tayari wilaya mbili za Meatu na Maswa zina huduma ya Mashtaka kwa ngazi hiyo na kusalia wilaya mbili za Busega na Itilima.
Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Simiyu
S. L P 169
Eneo/Mtaa -Malambo
Barua pepe:simiyu@nps.go.tz
Tovuti: www.nps.go.tz