Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Dar es Salaam
MKOA WA DAR ES SALAAM.
Mkoa wa Dar es salaam unapakana na Mkoa wa Pwani, upande wa Mashariki unapaka na Bahari ya Hindi. Mkoa huu una eneo la ukubwa wa kilomita za Mraba zipatazo 1,800; kati ya hizo, kilomita za mraba 1,350 ni eneo la nchi kavu ikijumuisha visiwa vinane vilivyopo katika eneo la bahari ya Hindi.
Idadi ya watu katika Mkoa wa Dar es salaam kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022 inaelezwa kuwa ni watu takribani milioni 5.6. Shughuli kuu za kiuchumi katika Mkoa wa Dar es salaam Biashara, Viwanda, Uvuvi, na Utalii. Makosa makubwa yanayotokea katika mkoa huo ni mauaji, Ubakaji, Dawa za Kulevya, Ulawiti na Nyara za Serikali.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Dar es salaam imeanzishwa mwaka 2018 na iko katikati ya Jiji la Dar es salaam ambapo tayari Wilaya zote tano zina huduma za Mashtaka.
Anuani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Dar es salaam
S. L P 71069
Eneo/Mtaa -Ohio
Barua pepe:daressalaam@nps.go.tz
Tovuti: www.nps.go.tz