Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Pwani

PWANI

Mkoa wa Pwani ulianzishwa rasmi mwaka 1972 na uko na wilaya nne ambazo ni Kibaha, Kisarawe, Mkuranga, Rufiji, Bagamoyo na Mafia. Shughuli kuu za kiuchumi katika Mkoa wa Pwani zimejikita katika maeneo makuu yafuatayo: Kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara, viwanda. Pia, Pwani ni maarufu kwa viwanda mbalimbali. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huo ni Kubaka, umiliki wa silaha kinyume cha sheria, unyanganyi wa kutumia Silaha na Mauaji.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Pwani inapatikana mtaa wa Mkoani Tumbi- A katika Manispaa ya Kibaha ambapo tayari Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imefungua Ofisi za Wilaya katika Wilaya za Bagamoyo, Chalinze na Mkuranga.

Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Pwani

S. L P 30393

Eneo/Mtaa -Mkoani A-Tumbi   

Barua pepe:pwani@nps.go.tz

Tovuti: www.nps.go.tz