Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Kigoma

KIGOMA.

Mkoa wa Kigoma una eneo la kilomita za mraba 45,075. Kati ya hizo, kilomita za mraba 36,523 ni nchi kavu na kilomita za mraba 8,552 ni eneo lililofunikwa na maji. Shughuli kuu za kiuchumi katika Mkoa wa Kigoma zimejikita katika maeneo makuu yafuatayo: Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Biashara, Utalii na Viwanda vidogo vidogo. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huu ni Uhamiaji Haramu, Mauaji, wizi na ukatili wa kijinsia.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Kigoma inapatikana mtaa wa Lumumba ndani ya Manispaa ya Kigoma Ujiji. Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imefungua Ofisi za Wilaya katika Wilaya za Kasulu na Kibondo.

 

Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Kigoma

S. L P 498

Eneo/Mtaa -Lumumba/Jengo la NHC  

Barua pepe:kigoma@nps.go.tz

Tovuti: www.nps.go.tz