Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Morogoro
. MOROGORO
Mkoa wa Morogoro ulianzishwa rasmi mwaka 1962 umegawanyika katika Wilaya saba ambazo ni Morogoro, Mvomero, Kilosa, Kilombero, Ulanga, Malinyi na Gairo. Mkoa una eneo la kilometa za mraba 73,039. Eneo hili ni sawa na asilimia 7.7 ya eneo lote la Tanzania Bara, kati ya eneo hili kilomita 2 2,240 ni eneo la maji. Shughuli kuu za kiuchumi katika mkoa huu ni kilimo, ufugaji, biashara, viwanda, madini, utalii na biashara. Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, idadi ya kaya za Mkoa wa Morogoro ni 489,688 zenye watu 3,197. Makosa makubwa ya jinai yanayojiri katika Mkoa huu ni mauaji, ubakaji, biashara ya madawa za kulevya, ujangili na wizi.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Morogoro inapatikana katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Morogoro
S. L P 6066
Eneo/Mtaa -Bomani \Jengo la RC
Barua pepe:morogoro@nps.go.tz
Tovuti: www.nps.go.tz