Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Kilimanjaro

KILIMANJARO

Mkoa wa Kilimanjaro ulianzishwa rasmi mwaka 1963 kwa Tangazo la serikali Na.450. Idadi ya watu ni 1,861,934 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi 2022. Shughuli kuu za kiuchumi ni Kilimo, Ufugaji, Viwanda na Biashara, Utalii.  

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Kilimanjaro inapatokana katikati ya Manispaa ya Moshi ambapo tayari Wilaya za Hai, Same, Rombo na Mwanga zina Ofisi za Mashtaka Wilaya huku ikisalia wilaya moja ya Siha. Makosa ya jinai makubwa yanayofanywa ni mauaji, ubakaji, dawa za kulevya na makosa ya ukatili wa kijinsia.

 

Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Kilimanjaro

S. L P 2401

Eneo/Mtaa -Mawenzi  

Barua pepe:kilimanjaro@nps.go.tz

Tovuti: www.nps.go.tz