Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Ruvuma
. MKOA-RUVUMA
Mkoa wa Ruvuma upo katika nyanda za juu kusini ukiwa na una jumla ya eneo la kilomita za mraba 64,393. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 mkoa huu una idadi ya watu 1,848,794. Shughuli kuu za kiuchumi katika Mkoa wa Ruvuma zimejikita katika maeneo makuu ya Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Biashara, Utalii na uchimbaji wa madini. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huo ni ubakaji, kulawiti, ujangili na kumiliki nyara za serikali.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Ruvuma iko mtaa wa CCM/Barabara ya Mbambabay katika Manispaa ya Songea. Kwa Upande mwingine, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ina ofisi za wilaya katika wilaya za Tunduru na Mbinga.
Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Ruvuma
S. L P 997
Eneo/Mtaa -CCM/Barabara ya Mbambabay
Barua pepe:ruvuma@nps.go.tz
Tovuti: www.nps.go.tz