Huduma Zetu
Huduma Zetu
Majukumu ya Ofisi
Mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya kusimamia uendeshaji wa mashtaka yote ya jinai katika Mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi yanatokana na Ibara 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Toleo la mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu Na. 9 cha Sheria ya Huduma za Mashtaka Sura ya 430. Mamlaka hayo haya yafuatayo:
- Kufanya uamuzi wa kufungua au kutofungua mashtaka;
- Kusimamia uendeshaji wa mashtaka yote ya jinai nchini isipokuwa yale yaliyo katika Mahakama za kijeshi;
- Kusitisha kesi iliyofunguliwa mahakamani na mtu au mamlaka yoyote kwa kuzingatia matakwa ya sheria;
- Kuchukua na kuendesha mashtaka yaliyofunguliwa mahakamani na mtu au mamlaka yoyote kwa kuzingatia matakwa ya sheria;
- Kukata rufaa au kufungua maombi au kujibu rufaa au maombi kwa niaba ya Jamhuri;
- Kusimamia na kuratibu shughuli za upelelezi pamoja na kuratibu shughuli zinazofanywa na vyombo vya upelelezi/chunguzi;
- Kuagiza chombo chochote kinachohusika na upelelezi wa makosa ya jinai kuendesha upelelezi kuhusiana na taarifa zenye mwelekeo wa jinai zilizofika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka;
- Kukagua magereza na mahali popote wanapohifadhiwa wahalifu kwa mujibu wa sheria;
- Kusimamia kazi za Jukwaa la Haki Jinai la Taifa, Mikoa na Wilaya;
- Kutoa ushauri wa kisheria kwa Mamlaka mbalimbali katika masuala ya Jinai;
- Kuendesha na kusimamia kesi zinazohusiana na utaifishwaji wa mali zinazohusiana na uhalifu;
- Kutoa miongozo mbalimbali kwa wadau wa Haki Jinai kuhusu upelelezi na uendeshaji wa mashtaka;
- Kuratibu mashauri yanayohusiana na uhamishwaji wa wahalifu kutoka ndani na nje ya nchi na kusaidia mamlaka za ndani na nje katika masuala ya Jinai;
- Kuelekeza na kushiriki kwenye utafiti wa kifo (inquests); na
- Kuunda kikosi kazi kwa ajili ya kuchunguza na kupeleleza suala mahsusi la kijinai kadri atavyoona inafaa.