Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Rukwa

. MKOA-RUKWA

Mkoa wa Rukwa ulianzishwa mwaka 1974 na una eneo la kilomita za mraba 27,765, kati ya hizo Kilomita za mraba 21,160 (76.21%) ni za nchi kavu na Kilomita za mraba 6,605 (23.79%) ni za maji. Mkoa wa Rukwa umegawanyika katika wilaya tatu ambazo ni Sumbawanga, Kalambo na Nkasi 

Kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2022, Mkoa wa Rukwa ulikuwa na Wakazi wapatao 1,540,519. Kiuchumi, wakazi wa Mkoa wa Rukwa wanajishughulisha na Kilimo, biashara, ufugaji, sekta ya utalii, madini, uvuvi, viwanda vidogo pamoja na biashara. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huo ni ubakaji, madawa ya kulevya, unyanganyi wa kutumia silaha, kupatikana na nyara mauaji na Wizi.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Rukwa inapatikana mtaa wa Mahakama Kuu katika Manispaa ya Sumbawanga.

 

Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Rukwa

S. L P 321

Eneo/Mtaa -Mahakama Kuu

Barua pepe:rukwa@nps.go.tz

Tovuti: www.nps.go.tz