Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Mbeya
Mbeya ni moja kati ya mikoa minne iliyopo katika Nyanda za juu Kusini mwa Tanzania Mkoa huu ulianzishwa mwaka 1961. Mkoa wa Mbeya una eneo la kilomita za mraba 63,617 kati ya hizo, kilomita za mraba 61,783 ni za nchi kavu na kilomita za mraba 1,834 ni eneo la maji. Kulingana na Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022 mkoa una idadi ya wakazi 2,343,754. Shughuli za kiuchumi katika mkoa huu ni kilimo, ufugaji, biashara na utalii. Makosa ya jinai makubwa yanayotokea mara kwa mara ni Mauaji, Ukatili wa kijinsia, Uhamiaji Haramu, Ujangili.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mbeya imeanzishwa rasmi mwaka 2018 baada ya kutenganishwa na iliyokuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ofisi yake ipo katikati ya jiji la Mbeya eneo la Mwanjela. Kwa upande wa Ofisi za wilaya, tayari ofisi za Wilaya zimekwisha funguliwa katika wilaya za Chunya, Kyela, Rungwe, Mbarali.
Anuani yaOfisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mbeya
S. L P 970
Eneo/Mtaa -Mwanjerwa
Simu: +255-252505038
Barua pepe:mbeya@nps.go.tz
Tovuti: www.nps.go.tz