Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Shinyanga

SHINYANGA.

Mkoa wa Shinyanga uko Kaskazini – Magharibi mwa Tanzania na Kusini mwa Ziwa Victoria ukipakana na mikoa ya Mwanza, Simiyu na Geita kwa upande wa kaskazini, upande wa mashariki Mkoa wa Simiyu, upande wa magharibi Mkoa wa Geita upande wa kusini Mkoa wa Tabora. Mkoa wa Shinyanga una ukubwa wa kilomita za mraba 18,555. Mkoa wa Shinyangauna idadi ya watu 2,241,299 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022.

Shughuli kuu za kiuchumi katika Mkoa wa Shinyanga ni kilimo, ufugaji, biashara, viwanda, madini na biashara. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huo ni mauaji, ubakaji, ulawiti na migogoro ya ardhi.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Shinyanga iko Katika jengo lake lililopo mtaa wa Pamba katikati ya Manispaa ya Shinyanga. Pia, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ina ofisi katika wilaya zote katika mkoa huu.

 

Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga

S. L P 635

Eneo/Mtaa -Pamba   

Barua pepe:shinyanga@nps.go.tz

Tovuti: www.nps.go.tz