Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Geita
GEITA.
Mkoa wa Geita ulianzishwa rasmi kwa Tangazo la Serikali namba 72 la tarehe 02 Machi, 2012. Mkoa huu ulitokana na sehemu ya Mikoa ya Mwanza, Kagera na Shinyanga. Mkoa huu una eneo au ukubwa wa kilometa za mraba 21,879. Ukiwa na wilaya tano ambazo ni Geita, Nyang‟hwale, Chato, Bukombe na Mbogwe. Kwa mujibu wa sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa una wakazi wapatao 2,977,608. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huu ni Mauaji, Ubakaji na Ujangili.
Wakazi wa Mkoa wa Geita wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji madini, biashara na Uvuvi.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Geita iko mtaa wa bomani katika Mji wa Geita.
Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Geita
S. L P 131
Eneo/Mtaa -Bomani
Barua pepe:geita@nps.go.tz
Tovuti: www.nps.go.tz