Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Mara

MARA.

Mkoa wa Mara una eneo la kilomita za mraba 30,150, kati ya eneo hilo kilomita za mraba 10,942 ni eneo la maji sawa na asilimia 36 na Kilomita za mraba 19,208 sawa na asilimia 64 ni eneo la nchi kavu.  Katika eneo la nchi kavu, Kilomita za mraba 9,452.34 sawa na asilimia 49.2 ziko katika Hifadhi za wanyamapori, ikiwemo Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mapori ya Akiba ya Ikorongo na Grumeti na Hifadhi za Jamii Grumeti na Ikorongo.

Mkoa umegawanyika katika wilaya sita ambazo ni Musoma, Butiama, Bunda, Serengeti, Tarime na Rorya. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Mkoa una watu wapatao 2,372,015. Uchumi wa mkoa huu unategemea zaidi kilimo ambacho uchangia kiasi cha 60% ya pato la Mkoa. Sekta nyingine ambazo uchangia kwenye uchumi ni mifugo, madini, uvuvi na utalii. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huo ni mauaji, ubakaji, ulawiti, ujangili, wizi na biashara ya madawa ya kulevya.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mara iko mtaa wa Lake Side manispaa ya Musoma.

 

Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mara

S. L P 823

Eneo/Mtaa -Lake Side/Jengo la RC    

Barua pepe:mara@nps.go.tz

Tovuti: www.nps.go.tz