Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Tabora

. TABORA.

Mkoa wa Tabora una eneo la kilomita za mraba 76,151, ambapo kilomita 34,698 (46%) ni hifadhi ya misitu na kilomita za mraba 17,122 (22%) ni hifadhi za Wanyama. Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, una idadi ya watu 3,391,679. Ukiwa na wilaya nane ambazo ni Tabora, Nzega, Igunga, Uyui, Urambo Sikonge na Kaliua. Shughuli kuu za kiuchumi katika Mkoa wa Morogoro ni kilimo, ufugaji, biashara, viwanda, Madini na Biashara. Makosa makubwa yanayotendeka katika Mkoa huu ni Mauaji, Ubakaji.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Tabora inapatikana mtaa wa Cheyo ndani Manispaa ya Tabora ambapo tayari Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imefungua Ofisi za wilaya katika Wilaya za Nzega, Kaliua, Urambo na Igunga.

Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Tabora

S. L P 199

Eneo/Mtaa -Cheyo A    

Barua pepe:tabora@nps.go.tz

Tovuti: www.nps.go.tz