Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

AHUKUMIWA KUNYOGWA MPAKA KUFA KWA KUUA.
07 Mar, 2025
AHUKUMIWA KUNYOGWA  MPAKA KUFA  KWA KUUA.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Sumbawanga yenye Mamlaka ya ziada imemhukumu  Sanyiwa Nyorobi  maarufu kwa jina la Ntemasho na kumpa adhabu ya kunyogwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kosa la Mauaji ya mkazi wa Sumbawanga Tiga Washa.

Hukumu hiyo imetolewa tarehe 4 Machi, 2025 na  Hakimu Mkazi mwenye Mamlaka ya ziada Mhe. Joseph Luambano baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.

Katika kikao cha Jinai namba 14637 cha mwaka 2024, Bw. Sanyiwa ni mkazi wa Kijiji cha Kilangawana kilichopo ndani ya Wilaya ya Sumbawanga , Mkoa Rukwa alikuwa anakabiliwa na shtaka la Mauaji  kinyume na kifungu cha 196 and 197 cha Sheria ya kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Rejeo la mwaka 2022.

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe 18 Desemba,2023 katika Kijiji cha Kilangawana kilichopo ndani ya Wilaya ya Sumbawanga Mkoa Rukwa ambapo inaidaiwa siku ya tukio mshtakiwa alivamia nyumbani kwa Tiga Washa ( Marehemu) na kumjeruhi kwa kumkatakata mapanga katika mwili na kupelekea kifo.