Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

AKUHUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA KWA KOSA LA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA
04 Mar, 2025
AKUHUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA KWA KOSA LA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA

Mahakama ya Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam imemhukumu Amosi Janus Nyitara 
 (23) kifungo cha miaka 03 jela baada ya kupatikana na dawa za  kulevya aina ya bhangi kiasi cha gramu 49.2.

Hukumu hiyo imetolewa tarehe 28 Februari, 2025 na  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Mhe. Vicky Mwaikambo  baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa kutoka upande wa Jamhuri.

Katika kesi hiyo ya Jinai namba 2685/2024, Bw. Amos  ambaye ni mkazi wa Mbagala Jijini Dar es salaam alikuwa anakabiliwa na shtaka la kukutwa na dawa za  kulevya aina ya bhangi gramu 49.2 kinyume na kifungu cha 17(1) (b) cha Sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya , (Sura ya 95 Rejeo la mwaka 2019)

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe 14 August, 2023 katika eneo la Kibonde Maji B Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam, alikutwa na madawa hayo isivyo halali.

Kesi hiyo imeendeshwa na jopo la Mawakili wa Serikali wawili kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka likiongozwa na Wakili Sabina Ndunguru Bundala akisaidiana na Nicas Kihemba.