Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

JELA MIAKA 19 KWA MAKOSA YA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU NA UTAKATISHAJI FEDHA
04 Sep, 2025
JELA MIAKA 19 KWA MAKOSA YA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU NA UTAKATISHAJI FEDHA

Mahakama ya Wilaya Mkoa wa Mbeya imemhukumu Steve Antony Kalimwa kutumikia kifungo cha miaka 19 gerezani kwa makosa ya Kujipatia Fedha kwa njia ya Udanganyifu na Kutakatisha fedha.

Hukumu hiyo imesomwa tarehe 29 Agosti,  2025 na Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Andrew Scout, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.

Katika kesi hiyo Na. 7312 ya mwaka 2025, Bw. Kalimwa mkazi wa Soweto Mbeya alitenda makosa hayo mnamo kati ya tarehe 13 Mei, 2024 na  21 Agosti, 2024.

Imethibibitika kwamba mnamo mwezi Januari,  2024 mshtakiwa akiwa nchini Oman alimtafuta mlalamikaji na kumwambia kwamba nchini humo kuna fursa mbalimbali za biashara ambazo zingemfaa kutokana na biashara alizokuwa anafanya. Mlalamikaji alishawishika na hivyo kumkubalia mshtakiwa na kumuagiza amnunulie viti 300, Televisheni, Chainsaw 50 na gari aina ya Toyota Landcruiser Hardtop.

Baada ya makubaliano hayo, mlalamikaji alianza kumtumia mshtakiwa fedha kwa viwango tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 13 Mei, 2024 hadi 21 Agosti,  2024 hadi kufikia TZS 93,270,000/=.

Akiwa anajiandaa kwenda kupokea bidhaa alizokubaliana na mshtakiwa, mlalamikaji alipata taarifa kwa njia ya ujumbe wa simu kuwa mshtakiwa amekamatwa Dar es salaam kwa kukutwana madini bandia ambapo alipofuatilia ilibainika kuwa taarifa hizo hazikuwa sahihi.

 Baada ya mshtakiwa kutafutwa na kukamatwa ilibainika kuwa hakuwa Oman na wala hakuwa na bidhaa alizoagizwa na mlalamikaji kwani fedha alizokuwa akitumiwa alikuwa akizitumia kwa matumizi binafsi ikiwemo kununua viwanja na kufungua duka la simu na vifaa vya simu.

Jumla ya mashahidi kumi wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi na vielelezo 11 vilitolewa.

 *Mtuhumiwa alijitetea mwenyewe
Mali na kifungo kwa Mshtakiwa, mahakama imetoa* amri ya kutaifishwa kwa viwanja viwili vilivyopo Ilomba - Mbeya na Magomeni, Sumbawanga-Rukwa.

Kesi hii imeendeshwa na Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mbeya