Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

"Tudumishe nidhamu na upendo mahala pa kazi" Kaimu Mwenyekiti.
23 Apr, 2024
"Tudumishe nidhamu na upendo mahala pa kazi" Kaimu Mwenyekiti.

[16:11, 22/04/2024] 568221: Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bi. Javelin Rugaihuruza amewataka Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kudumisha upendo na nidhamu mahala pa kazi ili  malengo ya Taasisi ambayo yamekusudiwa yaweze kufikiwa kwa asilimia mia ikiwa ni pamoja na kutoruhusu vishawishi vya rushwa kwani rushwa ni adui mkubwa wa haki.

Kaimu Mwenyekiti amebainisha hayo wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika tarehe 22 Aprili, 2024 Jijini Dodoma.

Kaimu Mwenyekiti amesema kuwa mkutano huo unalenga kujadili na kupitisha mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

"Tutumie vema kikao hiki ili tupate uelewa wa pamoja kuhusu masuala ya bajeti na mipango ambao tumejiwekea kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Tutumie muda wetu vizuri na kuweza kuidhinisha bajeti yetu kabla haijaenda kusomwa bungeni." Amebainisha hayo Kaimu Mwenyekiti.

Aidha Kaimu Mwenyekiti ameeleza kuwa kupitia bajeti hiyo itasaidia kutekeleza malengo mkakati ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ikiwa ni kuboresha maslahi ya watumishi, kuimairisha usimamizi wa utendaji kazi wao, kuboresha vitendea kazi na mazingira ya kazi ili kuleta tija na ufanisi katika utendaji kazi wao.

"Na kwa mwaka wa fedha huu endapo tutapitishiwa bajeti yetu itatusaidia kusogeza huduma za kimashtaka karibu na wananchi kwa kuongeza kufungua ofisi nyingine za Wilaya 15 pamoja na kuongeza majengo mapya matano katika Mikoa ya Kilimanjaro, Kigoma, Singida, Songwe na Lindi kwenye maeneo ambayo ofisi ina kiwanja na hati." Amefafanua hayo Kaimu Mwenyekiti.