Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

UJUMBE KUTOKA AFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA ZANZIBAR WAFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA MAHAKAMA YA TANZANIA
16 Aug, 2024
UJUMBE KUTOKA AFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA ZANZIBAR WAFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA MAHAKAMA YA TANZANIA

Ujumbe kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bara Bi. Bibiana Kileo pamoja timu nzima ya Kitengo cha TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bara wamefanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania Jijini Dodoma.

Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 14 Agosti, 2024 kwa lengo la kupata uzoefu wa kiutendaji ikiwa ni pamoja na kujifunza juu ya Mifumo ya TEHAMA kwa upande wa Mahakama namna wanavyoisimamia na kuiendesha.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar ameipongeza Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania kwa hatua waliyopiga katika uendeshaji wa mifumo ya TEHAMA kwani kupitia mafunzo hayo  wamepata elimu kubwa itakayowasaidia katika utendaji kazi wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA  Bw. Allan Machela kutoka Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania kwa niaba ya timu nzima ya TEHAMA wameushukuru ujumbe kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar kwa ujio wao  kutembelea Mahakama pamoja na kujionea namna mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi kwani ni njia mojawapo ya kuendelea kufahamiana pamoja na kukuza mashirikiano baina ya taasisi za Haki Jinai.