Habari

Imewekwa: Apr, 16 2021

WAHUKUMIWA MIAKA 20 JELA AU KULIPA KIASI CHA TSH.600,690,000/=

News Images

Mahakama ya Wilaya ya Ulanga imewahukumu washtakiwa Hassani Chikoko na Sudi Salum kwenda jela miaka 20 au kulipa faini kiasi cha Tsh. 600,690,000/= kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali.

Kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi Namba 6 ya mwaka 2019 iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Ulanga Mhe. Mhanusi, mahakamani hapo ilielezwa kuwa mshtakiwa Hassani Chikoko na mwenzake Sudi Salum walikutwa na nyara za serikali ambazo ni vipande 4 vya meno ya tembo, na hivyo kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini kiasi cha Tsh.600,690,000/= kwa kila mmoja.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri makahamani hapo pasipo kuacha shaka lolote.