Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20 AU KULIPA KIASI CHA TSH. 1,063,362,000/=
16 Apr, 2021
AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20 AU KULIPA KIASI CHA TSH. 1,063,362,000/=

Mahakama ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro imemuhukumu mshtakiwa Gerald Damiani Machege kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini kiasi cha Tsh.1,063, 362,000/=

Imeelezwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Ulanga Mhe. Matugwa Masimbi katika kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 22 ya mwaka 2019 kuwa mshtakiwa Gerald Damiani Machege alikamatwa baada ya kukutwa na vipande 15 vya meno ya tembo ambapo ni kinyume cha sheria.

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri pasipo kuacha shaka, na hivyo kupelekea mshtakiwa Gerald Machege kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini kiasi cha Tsh. 1,063,362,000/=

Kesi hiyo iliendeshwa na Mawakili wa Serikali Francis Malembo na Simon Mgonja