DPP ATEMBELEA MAGEREZA JIJINI DAR ES SALAAM.
DPP ATEMBELEA MAGEREZA JIJINI DAR ES SALAAM.
19 Nov, 2024

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu, afanya ziara ya siku tatu ya kutembelea magereza ya mahabusu Mkoa wa Dar es saalam kwa lengo la kuongea na kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo mahabusu na wafungwa ili kuweza kuzifanyia kazi kwa wakati.
Katika ziara hiyo, Bw. Mwakitalu aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Chalamila, Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Aretas Lyimo, viongozi ngazi ya mkoa wanaounda mnyororo wa Haki Jinai pamoja na Waendesha Mashataka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.
Ziara hiyo inafanyika tarehe 18-20 Novemba, 2024 Jijini Dar es salaam.