Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

NPS INASHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI KWA KUTOA ELIMU YA KISHERIA
28 Sep, 2026
NPS INASHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI KWA KUTOA ELIMU YA KISHERIA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, ametembelea banda la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) katika Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni, linalofanyika katika Viwanja vya Jamhuri, mkoani Morogoro.

Tamasha hilo linafanyika kuanzia tarehe 25 hadi 29 Agosti 2026, huku NPS ikishiriki kwa kutoa elimu na ushauri wa kisheria kuhusu haki jinai kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Akizungumza wakati alipowasili katika banda hilo na kupatiwa maelezo kuhusu majukumu ya Ofisi hiyo Mhe. Malima amesema NPS inapaswa kushiriki katika matukio mbalimbali yanayowakutanisha wananchi, kwa kuwa ni taasisi muhimu katika mnyororo wa haki nchini.

“NPS ni Ofisi nyeti inayopaswa kujulikana na umma, hivyo inatakiwa kujitokeza na kuonekana katika matukio yenye mikusanyiko ya watu ili kufahamisha umma kuhusu majukumu inayotekeleza na kutoa elimu kuhusu haki jinai,” amesema Mhe. Malima. 
 
Tamasha hilo limebeba kaulimbiu isemayo: “Utamaduni Wetu: Nguzo ya Maadili, Uchumi Jumuishi na Utaifa, AFCON 2027.”